Rais wa Marekani, Donald Trump amemtuhumu balozi wa Uingereza jijini Washington, Sir Kim Darrach baada ya kufichuliwa kwa baadhi ya nyaraka za siri akisema kuwa hatoshirikiana naye tena.

Katika mtandao wake wa Twitter, Trump pia amemtuhumu waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May akisema kuwa ”ni habari njema kwamba Uingereza itapata waziri mkuu mpya”.

Aidha, Sir Kim katika barua pepe zilizofichuliwa siku ya Jumapili aliutaja utawala wa rais Trump kama usiofanya kazi na usiojielewa.

Tamko la rais Trump la kukataa kushirikiana na balozi wa Uingereza nchini Marekani, Sir Kim Darroch, anamaanisha kwamba balozi huyo hatakiwi kuendelea kuwepo nchini mwake, hiyo ndio njia rasmi ambayo hutumiwa na serikali kumtimua mwanadiplomasia wa kigeni.

Hata hivyo, Uingereza iko katika hali ya sitofahamu ya kukubali shinikizo la Marekani la kumrudisha nyumbani balozi Kim, hatua itakayoifanya nchi hiyo kuonekana dhaifu ama kuwa na msimamo wa kumtetea balozi wake kwa kufanya kazi yake na kusema ukweli hatua ambayo huenda ikahatarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

 

Ujerumani yapuuza ombi la Marekani
Familia ya msaidizi wa Membe yaipigia goti serikali, 'Tusaidieni jamani kumpata Allan'