Khashoggi alitoweka tangu Oktoba 02 mwaka huu baada ya kuingia ubalozi mdogo wa Saudi Arabia Jijini Istanbul nchinil Uturuki.

Trump amesema kuwa amefanya mazungumzo ya simu kwa dakika 20 na Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman ambaye amemwambia kuwa hana taarifa yoyote kuhusu kilichomtokea Khashoggi.

Aidha, rais Trump amemtuma Waziri wake wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo mjini Riyadh kufanya mazungumzo na Mwanamfalme Salman kuhusu kutoweka kwa Khashoggi.

Khashoggi aliingia katika ubalozi mdogo Oktoba 2 ili kuchukua makaratasi yake aliyokuwa anayahitaji ili kumwezesha kufunga ndoa na mchumba wake, Hatice Cengiz, raia wa Uturuki ambaye alisubiri ndani ya gari nje ya jengo la ubalozi lakini hakumuona tena Khashoggi.

Pia Ufalme wa Saudia na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan walijadili juu ya kuunda kikosi kazi cha pamoja kuchunguza kupotea kwa Khashoggi, ambapo maafisa wa Uturuki wanaamini aliuawa na majasusi wa Saudia ndani ya Ubalozi.

Hata hivyo, Saudi Arabia imekanusha madai hayo kwa kusema kuwa hayana ukweli wowote na kuongeza kuwa Khashoggi aliondoka Ubalozini hapo kwa hiari yake.

Walinzi waeleza kwanini hawakuwa na bunduki wakati Mo Dewji anatekwa
Chadema yakanusha Mbowe na Mashinji kutofautiana