Rais wa Marekani, Donald trump amealikwa kushuhudia moja kwa moja pambano la masumbwi kati ya bondia Floyd Mayweather na mbabe Conor McGregor likatalofanyika Agosti 26 mwaka huu nchini humo.

Mshauri wa Maywether kwenye masuala ya biashara, Leonard Ellerbe amethibitisha kuwasilisha mualiko rasmi mezani kwa Rais Trump ili awe kati ya watu maarufu watakaokuwa katikati ya maelfu wanaotarajiwa kuhudhuria pambano hilo lililovuta umakini wa dunia ya masumbwi.

Trump ambaye kabla ya kuwa rais alikuwa mhudhuriaji mkubwa wa mapambano ya ngumi ikiwa ni pamoja na mieleka amekuwa na uhusiano wa karibu pia na Mayweather na McGregor.

Rais wa chama cha mapigano ya ubingwa wa kutumia ngumi na mateke kinachofahamika kama Ultimate Fighting Championship (UFC), Dana White amesema kuwa Rais Trump alionesha nia ya kutaka kuhudhuria pambano hilo tangu Julai mwaka huu.

Hata hivyo, Dana White ameeleza wasiwasi wake kama Trump atahudhuria tukio hilo kwani walinzi wanaweza kuchukua nafasi kubwa ya eneo ambalo lingeweza kubeba idadi kubwa ya watazamaji.

Mayweather na McGregor wanaendelea kulitangaza pambano lao katika miji mbalimbali huku pambano hilo likitajwa kuwa litavunja rekodi ya mapambano yote yaliyowahi kufanyika nchini humo kwa kuingiza kiasi kikubwa zaidi cha fedha. Pambano hilo limebatizwa jina la ‘The Money Fight’.

Christian Bella akumbuka msoto wa kujiunga na bendi ya Koffi , sasa anatafutwa
Picha: Majaliwa ahitimisha ziara yake mkoani Tabora