Mfuko wa maendeleo ya jamii Tanzania (Tasaf) umetumia sh 1.46 trillion kutekeleza mradi wa kunusuru kaya maskini katika kipindi cha kwanza cha awamu ya tatu ya mfuko huo.

Ambapo fedha hizo zimetumika katika kipindi cha kwanza cha awamu ya tatu ya mfuko huo kilichoanzwa kutekelezwa mwaka 2013 na na kukamilika desemba 2019.

Mfuko wa Tasaf ulianzishwa mwaka 2000 kwa kushilikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo lengo likiwa ni kupunguza umaskini kwa kutumia dhana ya ushirikishwaji jamii.

Akizungumza katika uzinduzi wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya Tasaf jijini Dar es Salaam leo Jumatatu ya Februari 17, 2020  Mkurugenzi mtendaji  Ladslaus Mwamanga amesema utekelezaji wa kunusuru kaya masikini umefanyika katika mamlaka ya serikali za mitaa 159 Tanzania bara huku Zanzibar ukifanyika kwenye wilaya zote.

Mwamanga amesema  zaidi ya kaya milioni 1.1 zenye watu milioni 5.2 ziliandikishwa kwenye mpango wa kupata ruzuku stahiki.

Aidha ametaja yaliyofanyiwa kazi ni kunusuru kaya masikini, ajira za muda kwa kaya masikini na kuongeza kipato kwa kaya masikini kupitia uwekaji akiba na kujimarisha kiuchumi

 

Makonda amwambia Magufuli '' Mkapa alinipa nauli''
Libya: Waziri aonya kutokea kwa mgogoro wa kifedha

Comments

comments