Treni ya mizigo iliyobeba shehena  ya ngano iliyokuwa ikitokea Dar es alaam kuelekea Mwanza imepata ajali usiku wa kuamkia jana mwaka huu eneo la Kola Manispaa ya Morogoro na kusabaabisha treni nyingine za abiria ambazo zilikuwa zinatoa Daresalam kwenda mikoa  ya kanda ya ziwa na nyingine kutoka Bara kwenda Daresaalm kushindwa kupita .

Akizungumza na waandishi wa habari  mkuu wa kituo cha Treni Morogoro Salvatory kimaro  amesema treni hiyo ilikuwa na injini namba C261 yenye jumla ya  mabehewa ishirini ambapo kati ya hayo mabehewa matano ya nyuma yaliacha njia na kuanguka  ambapo amesema chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika na hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu kama anavyobainisha

Aidha kimaro amefafanua kuwa kuhusu treni za abiria zilizokuwa zikitokea dar es salaam kuelekea kigoma, mpanda na mwanza zilifika mapema morogoro jambo ambalo limesaidia kubadilishwa kwa abiria waliotoka dar wakaingia iliyokuwa inatoka mwanza na wale wa mwanza wameendelea kwenye treni iliyokuwa ikitokea dar es salaam kuelekea mwanza.

Kwa ubande wao  baadhi ya wakazi wa morogoro wameiomba serikali  kuangalia kwa makini eneo kabla hayajatokea madhara kwa binadamu  kwani limekuwa likisababaisha ajali mara kwa mara.

Video: Serikali kukamilisha ujenzi wa barabra ya bilioni 500 Dodoma
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 14, 2019