Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), imeeleza kuwa, kuanzia mwaka ujao wa fedha 2018/2019 kutakuwa na mabadiliko katika kodi ya majengo ambapo, majengo ambayo hayajakamilika lakini yanatumiwa na watu yatatakiwa kulipiwa kodi.

Hatua hiyo ni tofauti na mfumo wa sasa ambapo kodi hutozwa kwa majengo yaliyokamilika tu.

Ameyasema hayo Mwelimishaji Mkuu TRA, Rose Mhendeka katika mkutano na waandishi wa habari leo.

iKiwa leo ni manzo wa wiki elimu kwa mlipakodi, Mhendeka amesema kuwa, awali kodi ya majengo ilikuwa katika sheria ndogo zinazosimamiwa na serikali za mitaa, lakini kwa sasa kodi hiyo ipo chini ya TRA na kwamba kuna uwiano katika  viwango vinavyolipwa.

Hivyo nyumba ya kawaida inalipwa TZS 10,000 na ghorofa ni TZSH 50,000 kwa sakafu lakini ghorofa inaweza kubadilika kutokana na thamani ya nyumba yenyewe.

”Awali awali watu hawakuwa wakilipa kodi kwa madai kuwa nyumba haijakamilika lakini unakuta wanakaa humo hadi miaka kumi”
Hivyo sasa wamebadili kigezo na watakuwa wanaangalia nyumba kukaliwa na watu badala ya kukamilika.

Aidha amesema kuwa sasahivi TRA iansimamia mapato yatokanayo na upangishwaji wa nyumba hivyo ni jukumu la kila muhusika kulipa kodi hiyo ambayo ipo kisheria.

Video: Serikali yalionya Gazeti la Tanzanite
Mrema adai Tahliso wanatumika