Klabu ya TP Mazembe imetangazwa kuwa bingwa wa ligi ya DR Congo (Linafoot) msimu wa 2019/20, huku ikiwa na michezo saba mkononi kukamilisha mzunguko wa ligi hiyo.

Kutokana na mlipuko wa COVID 19, Shirikisho la soka nchini humo (FECOFA) limeridhia kuufunga msimu wa ligi kuu 2019-20 kwa kuwapa ubingwa TP Mazembe wakiongoza kwa tofauti ya alama tano mbele ya AS Vita.

Maamuzi hayo ya FECOFA kuipa ubingwa TP Mazembe yamepingwa vikali na wadau wengi wa soka nchini humo wakiamini huenda AS vita yenye alama 48 nyuma ya 53 za TP Mazembe ingepata bahati ya kunyakua Ubingwa.

AS vita imecheza michezo 23 na TP Mazembe imecheza michezo 20 kabla ya ligi kusimamishwa. Maniema Union ipo nafasi ya 3 ikiwa na alama 46 ikicheza michezo 21.

Kwa maamuzi hayo TP Mazembe wanaendelea kuwa vinara kwenye orodha ya klabu zilizotwaa ubingwa wa ligi ya DR Congo (Linafoot) mara nyingi tangu ilipoanzishwa 1958.

TP Mazembe inakua imetwaa ubingwa huo kwa mara ya 18.

Kabla ya kutangazwa bingwa wa msimu huu, msimamo wa ligi ya ligi ya DR Congo msimu wa 2019/20 ulikua:

Manchester City waitega FC Bayern Munich
Madereva 23 wa Tanzania wazuiwa kuingia Kenya baada ya kukutwa na virusi vya corona