Mabingwa mara tano wa bara la Afrika klabu ya TP Mazembe wamepanga kujenga uwanja utakaochukua mashabiki 50,000 walioketi, kuanzia mwaka ujao 2020.

Rais wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu mjini Lubumbashi Moise Katumbi, ametangaza mpango huo leo Alkhamis, katika hafla maalum ya miaka 80, tangu kuzaliwa kwa klabu hiyo.

Miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla hilo iliyofanyika mjini Lubumbashi, Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino pamoja na Rais wa CAF Ahmad Ahmad, walihudhuria.

“Tumepata mkopo ambao utatuwezesha kujenga uwanja utakaochukua mashabiki 50,000, tumedhamiria kufanya ujenzi huo ili kutoa nafasi kwa mashabiki wetu kuishuhudia timu yao ikicheza uwanjani.” Alisema Katumbi.

“Kwa sasa tuna uwanja unaochukua mashabiki 22,000, muda unavyozidi kusogea tumebaini mashabiki wetu hawatoshi kwenye uwanja huo, na badala yake wanaishia kuishuhudia timu yao kupitia televisheni, lengo langu ni kuona kila mmoja anafika uwanjani kuishuhudia timu yake ikicheza.”

Kwa upande wa Rais wa FIFA Infantino amekiri kuvutiwa na mipango ya klabu hiyo ya DR Congo, na amesisitiza suala la kiongozi huyo kuendelea kupewa ushirikiano wa kutoka ili kufanikisha maendeleo ya soka nchini humo.

Pia akathibitisha usaidizi wa uwanja huo mpya wa TP Mazembe, kutoka FIFA ili kuonyesha ni vipi walivyoguswa na juhudi za Katumbi, ambaye siku zote amekua akidhihirisha kwa vitendo.

Image result for infantino and katumbiAhmad, Infantino na Katumbi baada ya mchezo wa jana uwanja wa TP Masembe

Jana Jumatano Ahmad, Infantino na Katumbi walishiriki katika mchezo maalum wa soka, ambao uliwashirikisha magwiji wa soka kutoka barani Afrika kama Samuel Eto’o na Kalusha Bwalya kwenye uwanja wa sasa wa TP Mazembe.

 

Video: Hotuba ya Profesa kabudi yaibua gumzo Kenya, Sumaye abwagwa uenyekiti Chadema
Mwakinyo, Mfilipino wapima uzito, tofauti yaonekana

Comments

comments