Ligi ya mpira kikapu nchini Marekani (NBA) inazidi kushika kasi ambapo katika dimba la Air Canada Center, Toronto Raptors imeibuka na ushindi wa alama 96-91 dhidi ya Detroit Piston.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali kwa timu zote mbili kila moja ikionesha kiwango bora kwenye harakati za kutafuta ushindi lakini bahati ikaangukia kwa Raptors kupitia kwa C.J.Miles aliyefunga alama 21 kwenye mchezo huo.

Jonas Valanciunas hakuwa nyuma kwenye mchezo huo kwa kupachika alama 17 na rebounds 16 ambazo ziliwasadia kupata ushindi katika mchezo wa leo.

Mchezaji mwingine wa Raptors ni Kyle Lowry ambaye alifunga alama 18 na DeRozan akafunga 17 na kuisadia timu yao kutokupoteza mchezo.

Januari 13, mwaka huu, Raptors wakiwa katika uwanja wa nyumbani walipoteza mchezo dhidi ya Golden State kabla ya kwenda kupoteza tena dhidi ya Philadelphia siku ya Jumatatu.

Raptors wameimarika wakiwa nafasi ya pili kwa kupata matokeo bora nyuma ya San Antonio ambao pia hutumia vizuri uwanja wa nyumbani, mpaka sasa Toronto haijapoteza michezo mfululizo wakiwa katika uwanja wa Air Canada Center tangu Januari 22 na 24 mwaka uliopita wakati walipopoteza dhidi ya Phoenix na Spurs.

Kwa upande wa Detroit Piston, Andre Drummond aliwezesha kupatikana kwa alama 25 katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo lakini Pistons hii ni mara ya saba wanapoteza katika michezo nane iliyopita.

Avery Bradley alifunga alama 19, Tobias Harris 12 na Langston Galloway akafunga alama 11 kwa Piston ambazo hazikusaidia kupata ushindi kwenye mchezo huo.

Bradley alianza katika Timu ya Pistons baada ya kukosa mchezo wa Januari 16 kutokana na kuumia hali ambayo ilimuweka nje ya kikosi kwa muda.

Kamati ya maadili yatangaza maamuzi dhidi ya wabadhilifu
Lipuli yaifuata Mbeya City