Kiungo kutoka Jamuhuri ya Czech Tomas Rosicky amebainika kuwa na matatizo ya goti, ambayo yatajhitaji upasuaji.

Kiungo huyo wa klabu ya Arsenal mwenye umri wa miaka 34, amebainika kuwa na matatizo hayo baada ya kufanyiwa vipimo mwishoni mwa juma lililopita.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha taarifa hizo mbele ya waandishi wa habari ambao walikusanyika kwenye mkutano maalum uliokua unazungumzia mchezo wa mwishoni mwa juma hili, ambapo The Gunners watacheza ugenini dhidi ya Crystal Palace huko Selhurst Park.

Endapo upasuaji huo utafanyika kwa mafanikio, Rosicky anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa majuma manane yajayo kabla ya kujiunga na wachezaji wenzake.

Rosicky, hakuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kilichokubali kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi ya nchini England mwishoni mwa juma lililopita, kwa kufungwa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya West Ham Utd.

Kikwete Na Lowassa, Mkono Kwa Mkono...?
Rafael: Van Gaal Hapedezwi Na Wachezaji Wa Brazil