Raia wa Togo wanapiga kura leo kuchagua Rais wa nchi hiyo, ikiwa ni nchi ya kwanza kwa mwaka 2020 kuchagua Rais huku zaidi ya nchi 20 za Afrika zikitarajiwa kufanya uchaguzi mwaka huu.

Serikali ya Rais anayetetea kiti chake kuongoza mhula mwingine wa nne, Faure Gnassingbe imepiga marufuku waangalizi wa asasi za kiraia pamoja na wa Kanisa Katoliki kuwa waangalizi wa uchaguzi huo.

Rais huyo aliye madarakani mwenye umri wa miaka 53, amekuwa akiliongoza taifa hilo lenye watu milioni nane tangu mwaka 2005, kufuatia kifo cha baba yake Gnassingbe Eyadema aliyeongoza kwa mkono wa chuma kwa miaka 38.

Serikali ya Togo ilikabiliwa na maandamano makubwa ya umma mnamo mwaka 2017 na 2018 ya kudai mwisho wa uongozi wa miongo mitano wa familia moja iliyoshindwa kuwainua raia wengi kutoka kwenye umaskini.

Serikali: Igeni kilimo cha nyanya Dodoma
Corona yazidi kusambaa Korea kusini, Iran, Japan