Timu ya taifa ya Marekani imetwaa ubingwa wa dunia kwa wanawake baada ya kukigalagaza kikosi cha Uholanzi kwenye mtanange wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Lyon uliopo nchini Ufaransa.

Mabao ya Marekani yaliwekwa kimiani na Megan Rapinoe na Rose Lavelle na kujihakikishia ubingwa huo kwa mara ya tatu pasi na kuruhusu nyavu zao kutikiswa na Uholanzi.

Hadi timu hiyo ya Marekani kuweza kufika katika fainali iliwalazimu kuwatoa Uingereza kwa kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezeka julai 2 mwaka huu nchini Ufaransa.

Aidha, hii ni mara ya tatu kwa Marekani kunyakua taji hilo la dunia kwa upande wa wanawake ambapo iliwahi kufanya hivyo mnamo mwaka 1991, 1999, 2015 pamoja na mwaka huu.

Uholanzi nayo ilikua ikicheza fainali yao ya pili huku wapinzani wao wakicheza fainali yao ya tatu ya kombe hilo la dunia huku mshindi wa tatu katika michuano hiyo ni Sweden ambao waliwafunga Uingereza kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Allianz Riviera katika jiji la Nice.

Marekani wameweza kubeba taji hilo huku wakiwa na rekodi ya kuifunga timu ya taifa ya Thailand kwa kipigo kizito cha mabao 13-0 katika michuano hiyo.

Watu saba wafariki dunia katika ajali iliyotokea Singida
40 ya Dani Alves yatimia

Comments

comments