Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani ambaye ametembelea Kenya amesisitiza umuhimu wa kuwepo vyombo huru vya habari katika kukuza demokrasia na kutaka serikali zisiminye uhuru wao.

“Tunaamini kuwa lazima hatua fulani zichukuliwe nchini Kenya na pia yawepo marekebisho ya hatua zilizochukuliwa, kama vile kufunga vituo vya televisheni na kutishia uhuru wa mahakama,” amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson.

“Nafahamu kuwa Kenya inatizama masuala haya kwa umakini wa hali ya juu. Vyombo vya habari huru binafsi ni muhimu katika kulinda demokrasia na kuwapa wananchi wa Kenya imani na serikali yao,” ameongeza.

Amezungumza hayo kufuatia Serikali ya Kenya kuvifungia vituo vitatu vya televisheni mwezi Januari 2018, siku ambayo Odinga alijiapisha,.

Serikali ilikiuka amri ya mahakama iliyokuwa inataka vituo hivyo vifunguliwe, ambavyo vilipanga kuonyesha kujiapisha kwa Odinga.

Wakati huohuo Waziri Tillerson ameshindwa kuhudhuria shughuli alizokuwa amepangiwa kuzifanya Jumamosi katika siku ya pili ya ziara yake nchini Kenya kwa kuwa hajisikii vizuri.

Tillerson, miaka 65, yuko katika siku ya nne ya ziara yake ya kwanza ya kidiplomasia katika bara la Afrika.

Manara kuhama CCM, Liverpool ikiifunga Manchester mchuano wa leo
Rais aamua kujiuzulu kwa tuhuma zinazomkabili