Wakati kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kikijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya  Misri leo jioni, utakaopigwa nchini Misri, uongozi wa Stars kupitia meneja wake, Dany Msangi umesema baadhi ya wachezaji waliotemwa wapo mbioni kurejea nchini.

Akiongea na kituo kimoja cha redio nchini  jana, Msangi amesema jumla ya wachezaji tisa ambao wametemwa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emanuel Amunike tayari wamekatiwa tiketi za ndege ili safari ya kurejea nchini ianze.

Kuhusu mchezo wa leo wa kirafiki baina ya Tanzania na Misri, Msangi amesema maandalizi yanaendelea vizuri katika nchi hiyo ambapo mtanange wa leo jioni huenda ukawa kipimo sahihi kwa Amunike kujua kikosi chake kikoje na kipi aongeze.

Ikumbukwe siku chache zilizopita, kocha huyo alitangaza kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya AFCON mwezi huu ambapo  wachezaji alioenda nao Misri kisha wakatemwa ni Abdi Banda, Shaban Idd Chilunda, Fred Tangalu, Suleiman Salula, Claryo Boniface, Miraji Athumani, David Mwantika, Kelvin John, na Shiza KIchuya.

2018-2019: Pato la Mtanzania laongezeka kwa Sh 100,000
Miley Cyrus aomba radhi kwa kuiponda Hip-Hop