Msanii wa bongo fleva nchini, Khalid Mohamed maarufu kwa jina la TID amepigwa na watu aliowaita kuwa ni majambazi na kupelekea kuumizwa sehemu ya jicho, ambapo video iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii hapo jana ilimuonyesha akiwa anapigwa na watu ambao bado hawajajulikana ni kina nani.

TID aliposti picha katika ukurasa wake wa Instagramu ikimuonyesha akiwa ametapakaa damu na kuandika kuwa ”Washamba bwana wakiona tu Unasikika wanaamua kukupiga hivi I’ts so sad Jambazi anaweza kukufanyia chochote yeye jambazi na yuko na back up za kijambazi”aliandika TID.

Amesema kuwa kwasasa anaendelea vizuri japo jicho lake lina maumivu kwani alichomwa na kitu chenye  ncha kali sehemu ya jicho, ambapo daktari amemwambia arudi tena hosipitali baada ya siku tatu kwaajili ya uchunguzi zaidi wa jicho lake.

Ameongeza kuwa kwasasa ametoa taarifa polisi kwaajili ya ulinzi wake na usalama kwa kile ambacho kimetokea baada ya wale aliopigana nao kutishia kumfyatulia risasi.

TID ambaye anatarajia kutoa burudani katika ukumbi wa fortyforty uliopo jijini Dar es salaam amesema kuwa onyesho hilo litakuwepo kama lilivyopangwa na hakuna ambacho kitabadilika kutokana na tatizo lililotokea na amewataka mashabiki wake wahudhurie na ratiba iko palepale.

Aidha, mwanamuziki huyo amekiri kuwakosea mashabiki wake baada ya tukio hilo kwani hakukuwa na sababu ya yeye kupigana na amewaomba radhi mashabiki kwa kitendo kilichotokea.

TASAF Njombe yawawezesha walengwa
Mzee wa miaka 70 asukumwa ndani kwa kulipiga mawe gari la Rais

Comments

comments