Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imewatoa hofu wanafunzi baada ya kumaliza kidato cha nne wanaotamani kujiunga na chuo hicho, kuwa hawaangalii hesabu pekee, wanaweza kusoma ngazi ya cheti cha awali wakiwa na D nne kwenye masomo yao yeyote isipokuwa ya dini.

Chuo hicho kinachofundisha masomo ya Uhasibu, Ununzi na Ugavi, usimamizi wa biashara, uongozi wa raslimali watu, masoko na uhusiano wa umma, uhasibu wa umma na fedha pamoja na nyanja nyingine za biashara pia kinatoa ushauri na kufanya tafiti mbalimbali.

Mkuu wa Masoko na Uhusiano kwa Umma, katika chuo hicho, Lilian Mpanju amesema kumekuwa na wanafunzi wengi ambao wanaogopa kujiunga kwa kujua wanaangalia somo la hesabu kwanza.

” Nazidi kuwasisitiza wazazi kuwapa fursa watoto kusoma, unakuta mwanafunzi hajafaulu vizuri kwenda ‘A – level’ na amerisiti na kukata tamma, kunanafasi ambapo agemleta na kuanzia ngazi ya awali atimize ndoto zake” Amesema Lilian

Bofya hapa kutazama