Mtandao wa kijamii wa Facebook umeporoka thamani yake kwa $58 bilioni kati ya Jumatatu na Ijumaa kutokana na kashfa ya kushindwa kulinda taarifa za watumiaji zaidi ya milioni 50.

Kutokana na uzembe wa wataalam wa mtandao huo, taasisi inayojishughulisha na uchambuzi wa masuala ya kisiasa iliweza kuingilia taarifa za siri za watumiaji zaidi ya milioni 50 wa mtandao huo.

Kashfa hiyo ya kisiasa iliyoikumba Facebook ilimlazimu mmiliki wa mtandao huo, Mark Zuckerberg kuomba radhi kwa watumiaji akiahidi kutojirudia tena.

Hata hivyo, makampuni hasimu ya mtandao huo yaliweka jitihada za kuchochea kashfa hiyo zilizosababisha makampuni kadhaa kuondoa hisa zao pamoja na matangazo.

Hisa za mtandao huo zilishuka kutoka $176.80 Jumatatu asubuhi hadi $159.30 siku ya Ijumaa jioni.

Kufikia Februari mwaka huu, hisa za Facebook zilipanda hadi $190 kutokana na ukuaji wa kiutawala na kuaminika, lakini wiki hii ziliuzwa hadi $38 kila moja na kuipa kampuni hiyo thamani ya $104 bilioni.

Magazeti ya Tanzania leo Machi 26, 2018
Mbaroni kwa kubaka wakionesha ‘Live’ Facebook