Albam mpya ya Lil Wayne ‘Tha Carter V’ inatarajia kushika nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard 200 wiki ijayo, kwa mujibu wa Daily Double.

Hii inatokana na mafanikio iliyoyapata kwenye wiki yake ya kwanza ikiwa inakimbilia mauzo ya 475-525,000 kwenye mtandao, ambayo ni sawa na kati ya nakala za kawaida 165,000 – 180,000.

Nyimbo za albam hiyo zimefanikiwa kusikilizwa zaidi ya mara 49.5 milioni ndani ya saa 24 kwenye Spotify, kwa Marekani pekee na kuweka rekodi ya kuwa albam ya pili kusikilizwa zaidi kwenye mtandao huo kwa muda mfupi ikiwa nyuma ya Scorpion ya Drake iliyopita 80.5 milioni ndani ya siku moja.

Hadi sasa, Tha Carter V imeweza kupata streams zaidi ya milioni 100 kwenye mtandao huo, kwa mujibu wa Chart Data.

Hata hivyo, mafanikio ya Tha Carter V yako nyuma sana ya mafanikio aliyoyapata kwenye Tha Carter IV miaka saba iliyopita ambapo iliuza nakala 964,000 katika wiki ya kwanza kabla ya kuanzishwa kwa ‘streaming’.

Tha Carter V imeachiwa rasmi Ijumaa usiku kukata kiu ya miaka saba ya mashabiki wake. Ndani wameshirikishwa Kendrick Lamar, Nicki Minaj, Travis Scott, Snoop Dogg, na marehemu  XXXTentacion.

Diamond arejea kuokoa maisha ya Hawa, ampa mamilioni
Nafasi za ajira kutoka makampuni 10 Tanzania