Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Tanzania (TFF) limetangaza kusitisha mkataba na kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike.

Taarifa iliyotolewa na TFF imesema kuwa kuwa Amunike amekubaliana na TFF kusitisha mkataba wake, ambapo shirikisho hilo pia limesema kuwa litatangaza kocha wa muda atakayekiongoza Kikosi cha Timu ya Taifa katika mechi za CHAN.

Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Tanzania maarufu kama ‘Taifa Stars’ mwezi Aprili mwaka 2018, na kufanikisha kuingoza kufuzu kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya miaka 39.

Aidha Amunike amekuwa akilaumiwa na baadhi ya mashabiki kwa namna anavyoteua wachezaji na kupanga kikosi, ambapo katika mashindano yanayoendelea nchini Misri, Tanzania ilitolewa baada ya kupoteza michezo yote ya makundi.

Tanzania ndiyo timu iliyofanya vibaya zaidi katika mashindano hayo kitakwimu kwenye hatua ya makundi, ambapo imefungwa jumla ya magoli nane na kufunga mawili, hivyo wamemaliza wakiwa na uwiano wa magoli -6.

 

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 9, 2019
Video: TBA yaja na utaratibu mpya wa malipo

Comments

comments