Kamati  ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeunda Kamati ya Maendeleo ya Miradi ili kusimamia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vituo vya michezo vya Kigamboni, Dar es Salaam na Tanga.

Kabla ya kuunda Kamati hiyo, Kamati ya Utendaji ilipokea taarifa ya maandalizi ya utekelezaji wa miradi hiyo kwenye kikao chake kilichofanyika Februari 18, 2020 jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni QS Lucy Mzengi (Mwenyekiti), Mhandisi Hersi Said, Mhandisi Hamad Ramadhan, na Mhandisi Charles Adrian.

Kikao hicho cha kawaida vilevile kilipokea Taarifa ya Rais, Taarifa ya Utekelezaji ya Sekretarieti, Utekelezaji wa Mpango Mkakati wa TFF (Strategic Plan) kwa mwaka 2020 na kufanya uteuzi wa Kamati ndogo za TFF.

Wajumbe walioteuliwa katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ni Mwanasheria Elias Mwanjala (Mwenyekiti), Said Soud (Makamu Mwenyekiti), Zakaria Hans Poppe, Issa Batenga, Wakili Msanifu Kondo, na Said George.

Kamati ya Fedha na Mipango ni Athumani Nyamlani (Mwenyekiti), Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Pascal Kihanga, Maxmillian Tabonwa, Paul Bilabaye, Allen Mrindoko, Evans Mgeusa, na Seif Muba.

Kamati ya Mashindano ni Ahmed Mgoyi (Mwenyekiti), Saloum Chama (Makamu Mwenyekiti), James Mhagama, Patrick Kahemele, Fortunatus Kalewa, Shafih Dauda, Sarah Chao, Said Tully, na Ali Kamwe.

Kamati ya Ufundi ni Vedastus Lufano (Mwenyekiti), Mrisho Bukuku (Makamu Mwenyekiti), Ibrahim Masoud, Ally Mayay, Michael Bundala, Jumbe Menye,na Edibily Lunyamila.

Kamati ya Mpira wa Vijana ni Khalid Abdallah (Mwenyekiti), Lameck Nyambaya (Makamu Mwenyekiti), Mohamed Aden, Nassib Mabrouk, Salim Kibwana, Vicent Majili, Kenneth Pesambili, Nicky Magarinza, na Philip Alando.

Kamati ya Waamuzi ni Soud Abdi (Mwenyekiti), Israel Nkongo (Makamu Mwenyekiti), Zahra Mohamed, John Kanyenye, na Samwel Mpenzu.

Kamati ya Mpira wa Wanawake ni Amina Karuma (Mwenyekiti), Mia Mjengwa (Makamu Mwenyekiti), Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Zena Chande, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, na Zabibu Juma.

Kamati ya Habari na Masoko ni Steven Mnguto (Mwenyekiti), Osuri Kosuri(Makamu Mwenyekiti),Cyprian Kuyava, Mgaya Kingoba, Dk. Omar Saleh, na Saleh Ally.

Kamati ya Tiba ni Dk. Paul Marealle (Mwenyekiti), Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Norman Sabuni, Dk. Lisobina Kisongo, Dk. Eliezer Ndama, Dk. Billy Haonga, na Dk. Violet Lupondo.

Kamati ya Futsal na Beach Soccer ni Blassy Kiondo, Isaac Munisi, na Didas Zimbihile.

Kamati ya Leseni za Klabu ni Wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), Sunday Kayuni, George Mayawa, na Tumaini Mringo.

Kamati ya Rufani za Leseni ni Dk. Damas Ndumbaro (Mwenyekiti), Dk. Alex Mgongolwa (Makamu Mwenyekiti), Charles Matoke, David Kivembele, na Robert Selasela.

Kila mwaka wanawake 50 hushambuliwa kwa tindikali
Ndayiragije: Nitaiandaa vyema Taifa Stars