Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) limesaini makubaliano ya miaka mitatu ya ushirikiano na Shirikisho la Soka nchini Hispania kwa lengo la kuisadia Tanzania kusonga mbele.

Katika jitihada za uongozi wa TFF ulioingia madarakani Agosti, 2017 kuhakikisha unaboresha soka nchini, umepiga hatua nyingine baada ya Rais Karia kutua nchini Hispania na kusaini makubalinao ya ushirikiano na Ligi Kuu ya huko maarufu La Liga

Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imesema kuwa pande hizo mbili yaani TFF na La Liga zimesaini makubaliano ya miaka mitatu kushirikiana kwa pamoja kuendeleza soka la Tanzania.

Aidha, pande hizo mbili zimesaini makubaliano hayo, jana Juni 18,2018 kwenye makao makuu ya La Liga yaliyopo jijini Madrid nchini Hispania, ingawa haijawekwa wazi pande hizo zitashirikiana kwenye maeneo gani zaidi.

Hata hivyo, Rais Wallace Karia wa TFF amekutana na Rais Javier Tebas wa La Liga baada ya kutoka nchini Urusi ambapo alihudhuria ufunguzi wa fainali za Kombe la Dunia zilizoanza Alhamisi iliyopita Juni 14.

Mbuga tatu za wanyama Tanzania zatajwa kuwa bora zaidi Afrika 2018
Mbowe aweka hadharani kinachomsumbua