Newcastle imeanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, 28, baada ya Bayern Munich kubadili nia ya kumpatia mkataba wa kudumu nyota huyo wa kimataifa wa Brazil. (Mundo Deportivo – in Spanish).

  • Arsenal na Tottenham wanang’ang’ania kumsajili kwa mkataba wa bila malipo kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 31, ambaye mkataba wake Stamford Bridge unakamilika msimu huu. (Telegraph).
  • Manchester City wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsaka kinda wa Ajax Sontje Hansen, 18, ambaye alishinda tuzo ya Golden Boot katika kipute cha kombe la dunia kwa wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 17 msimu uliopita. (Goal).
  • Ripoti kutoka Ujerumani zinadai kuwa meneja wa Liverpool Jurgen Klopp alifanya mazungumzo mazuri na mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner wakati wa Pasaka,(Sport Bild).
  • Baada ya Barcelona kutangaza nia ya kumuuza mshambuliaji wao raia wa Ufaransa Ousmane Dembele vilabu kadhaa barani ulaya kama Arsenal, PSG na Juventus vimeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo (Mundo Deportivo).
  • Wolves huenda wakamnunua kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Joao Palhinha, 24. (Mirror).
Kagera Sugar kuweka kambi Kagera
Australia yaanza jaribio la kwanza chanjo ya Corona

Comments

comments