Inasemekana mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha (26), bado ana matarajio ya kuondoka Crystal Palace ambapo uhamisho wake huenda ukafanyika  katika dirisha la usajili litakapofunguliwa tena Januari Mwakani.

Manchester United inapania kumsajili mshambulizi wa Juventus wa miaka 33 Mcroatia Mario Mandzukic na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa na Barcelona, Ousmane Dembele, 22, Januari Mwakani.

Maafisa wa matibabu wa mshambuliaji wa Newcastle na Uingereza Andy Carroll, wanahofia mchezaji huyo huenda asiingie uwanjani hadi baada ya Krismasi japo anaendelea kupata nafuu kufuatia jeraha la mguu alilopata.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema meneja wa sasa wa Rangers na nahodha wa zamani wa Reds Steven Gerrard ndiye atakayemrithi atakapoamua kuondoka Anfield.

Sevilla iko tayari kumuachilia kiungo wa kati wa Ureno Rony Lopes mwezi January huku Newcastle ikimfuatilia mkufunzi huyo wa zamani wa Manchester City wa miaka 23.

Gianni Infantino kula sahani moja na wabaguzi wa rangi

Mshambuliaji wa zamani wa Celtic na Manchester United Henrik Larsson huenda akapewa wadhifa wa Southend, kutokana na hali ngumu ya kiuchumi inayomkabili na ukosefu wa tajiriba ya ukufunzi wa vilabu vya Uingereza ambao imekua changamoto kwake.

Misri yapata kocha mpya

 

Francois Zahoui abeba jukumu la kuivusha Les Fauves
Vyombo vya habari vyamtabiria mabaya Ole Gunnar Solskjaer

Comments

comments