Mtandao wa kutokomeza ndoa za utotoni Tanzania (TECMN) unaojumuisha taasisi zisizo za kiserikali zaidi ya 50 wameipongeza Mahakama ya rufani kwa kufanya mabadiliko ya kifungu cha 13 na 17 katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Mtandao huo umekuwa ukifanya jitihada na mikakati mbalimbali ya uhamasishaji na uelimishaji juu ya athari za ndoa za utotoni, ambapo wamekuwa wakifanya tafiti tofautitofauti kuonesha ukubwa wa tatizo la ndoa za utotoni huku sababu kubwa ikiwa ni umaskini, mila na desturi,pamoja na na sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Hata hivyo Tanzania ni moja ya nchi zenye kiwango cha juu cha ndoa za utotoni duniani kwa mujibu wa takwimu za UNICEF za kati ya mwaka 2010 na 2017 Tanzania ni ya tatu  kwa kuwa na viwango vya juu vya ndoa za utotoni baada ya Sudani Kusini na Uganda.

Aidha madai yaliyopelekwa mahakami na Rebeca Gyumi ya kupinga sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ambapo tarehe 23 ya mwezi Octoba 2019 mahakama ya rufani Tanzania ilikubalia na maamuzi yaliyotolewa na mahakama kuu ya Tanzania kubadilisha vifungu hivyo kwakuwa ni vya kibaguzi.

Hata hivyo mtandao huo umeelezea athari za ndoa za utotoni ikiwa ni pamoja na kupoteza fuursa za elimu na ujuzi wakazi, kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi huku wengi wao wakinyanyasika kisaikolojia kimwili na kijinsia

Meya wa Arusha ajiunga CCM baada ya kupokea vitisho
Video: Hakuna wanawake wanaojifungulia chini Muhimbili

Comments

comments