Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekabidhi leseni za kufanya huduma ya kutoa habari kwa njia ya mtandao kwa Online TV ikiwemo Dar24 Media, Online Redio na Blogs ambazo zimekamilisha usajili.

Akizungumza katika utoaji wa leseni hizo, Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Mhandisi James Kilaba amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na lina lengo la kuzuia uanzishwaji holela wa Online TV, Online Radio na Blogs ambao unaweza kusababisha madhara kwa jamii.

“Jambo la kwaza tunazuia uanzishwaji holela wa vyombo vya habari mtandaoni usiokidhi viwango vinavyotakiwa, ikumbukwe kwamba umiliki wa vyombo vya habari bila tozo unaweza ukaleta utitiri wa vyombo hivi na ikawa changamoto katika usimamizi na kwa jamii,”amesema Mhandis Kilaba

Aidha, amesema kuwa lengo la pili ni kuleta ushindani sawa, hivyo sio vyema vyombo vya habari vinavyotumia majukwaa mengine kulipia leseni wakati vyombo vya mtandaoni havilipii gharama yoyote.

Hata hivyo, Mhandisi Kilaba ameongeza kuwa jambo la tatu ni kutambua watu wenye nia safi ya kutoa huduma hiyo ya maudhui mtandaoni kwa jamii.

Mhandisi James amezitaka Online TV, Online  pamoja na blogs mbalimbali kuendelea kujitokeza kwa ajili ili waweze kufanya kazi kwa uhuru huku akidai hatua hiyo itafungua milango ya kibiashara kwa blog na online tv.

 

Magazeti ya Tanzania leo Mei 26, 2018
Bocco atamba kuiangamiza Majimaji FC