Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Francis Mihayo ametoa ufafanuzi wa kina juu ya usajili wa mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram na Twitter ambayo inajihusisha kurusha video kama namna ya kuhabarisha jamii.

Amesema kuwa endapo mtu atatumia mitandao hiyo ya kijamii kurusha vipande vya habari kwa video atakuwa ameugeuza mtandao huo kuwa televisheni ya mtandaoni.

Hivyo amewataka wamiliki wa akaunti hizo kutoa taarifa mamlaka ya mawasiliano ili waweze kusajiliwa kama watoa huduma mtandaoni.

”Kurusha clips ambazo zina video kwa maana kwamba unaugeuza facebook kama platform kama eneo la kutuma habari za televisheni mtandaoni hiyo na yenyewe unatakiwa utoe taarifa mamlaka ya mawasiliano waweze kukusajili kama mtoa huduma mtandaoni”. Mihayo.

Ameongezea kuwa usajili huo hautahusiana na wamiliki wa mitandao ya kijamii ambao watatumia mitandao hiyo kurusha picha.

Aidha amesisitiza kuwa sheria imeelekeza wamiliki wa akaunti ni lazima wawe makini kuangalia ni kitu gani ambacho kinachangiwa na wafuasi wao au ni kitu gani kinachotumwa na wafuasi wao au yeye mwenyewe anachokiweka kwani sheria imeeleza pia ni adhabu ipi itatolewa kwa mtu atakayefanya makosa mtandaoni.

TCRA Imetangaza kuwa kuanzia Juni 11 – 15, 2018 watoa huduma wote wa mitandaoni wanatakiwa kusitisha zoezi hilo mpaka pale watakapojisajili na endapo watakiuka basi haitasita kumchukulia hatua.

 

Zitto ampa tano Upendo Peneza
Video: Ninayo mengi zaidi ya kumueleza JPM- Mzee Mashaushi