Kufuatia habari iliyotolewa na Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akidai kusikitishwa na kauli za Diamond alizozitoa dhidi ya Naibu wake, Juliana Shonza, hivyo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kamati yake ya maudhui inafuatilia kiundani mahojiano ya mwanamuziki huyo na kuyatolea ufafanuzi wa kina.

Ambapo Diamond Platinumz moja ya maneno ya kashfa aliyozungumza dhidi ya Shonza amesikika akisema, Waziri huyo amekurupuka kufanya maamuzi ya kuwafungia wasanii kazi zao za muziki, ili hali muziki huo ndio unaowasaidia wasanii kuendesha maisha yao na familia zao.

Diamond alizungumza hayo katika kipindi cha The playlist kinachofanywa na mtangazaji Lily Ommy katika radio ya Times FM.

Hata hivyo Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Andrew Kisaka amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa mahojiano hayo yamefanyika katika kituo chao wanachokisimamia.

Kisaka amefafanua kuwa kiutaratibu wao wanaangalia zaidi chombo ambacho wamekipa leseni na kwamba, masuala mengine yatashughulikiwa na mamlaka nyingine.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo DKt. Harrison Mwakyembe amesema si busara kwa Diamond kushindana na serikali endapo ana ushauri wowote ni vema akauwasilisha kwa njia sahihi na si kumshambulia Naibu Waziri kwa dharua na kejeli.

Lipumba aunga mkono jitihada za JPM na serikali ya awamu ya 5
Marekani yaweka vikwazo Sudan Kusini