Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini TASAF mkoani Njombe umefika vijijini na kutoa elimu kwa walengwa wa mradi huo ikilenga kujua umuhimu wa kujiwekea akiba katika vikundi vyao kwa ajili ya kutatua matatizo ya siku za usoni.

Hii inakuja baada ya wawezeshaji kupatiwa mafunzo ya kwenda kuwafundisha walengwa hao ambapo katika halmashauri ya wilaya ya Njombe msafara wa wawezeshaji hao umefika katika vijiji vya Ibumila na Itunduma na kutoa elimu hiyo kwa walengwa hao.

Mwezeshaji wa TASAF kutoka halmashauri ya wilaya ya Njombe, Majula Mujungu amesema kuwa kikubwa wamewafikia wananchi hao na kuwaelekeza namna ya kuweka akiba, kutatua migogoro katika vikundi vyao pamoja na kutoa elimu ya uongozi katika vikundi vya akiba ambavyo vimeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia kupitia Tasaf.

Nao wananchi kutoka katika kijiji cha Itunduma, Twilumba Nyagawa na Suzana Bundala wamesema kuwa hatua ya serikali kuwapa mafunzo hayo itawasaidia sana kuepukana na changamoto zinazoweza kuwakumba baada ya kushindwa kuweka akiba, kushindwa kutatua migogoro katika vikundi pamoja na mifarakano itakayotokana na kutokuwa na elimu ya uongozi bora katika vikundi vyao.

Kwa upande wake, Afisa malalamiko kutoka TASAF, Makwinja Dismas Yusuf amesema kuwa kila mradi huwa na mwanzo na mwisho hivyo wameona ni lazima kuanzisha vikundi ambavyo vitawasaidia walengwa hao hata pale mradi utakapofikia ukomo.

Elimu hiyo ya kuwajengea uwezo wanufaika wa TASAF katika vijiji mbalimbali inafanyika kwa siku mbili kwa viongozi wa vikundi mbalimbali ili kuwawezesha kuendesha vikundi vyao wakiwa na uelewa ambao utakuwa na maslahi kwa walengwa wote

 

Mambo 10 usiyofahamu kuhusu ubongo wa binadamu
TID akiri kuwaangusha mashabiki, 'Naombeni mnisamehe sana'

Comments

comments