September 19, 2016 kituo cha TV cha CNN Kiliripoti kuhusu muigizaji mwenye mvuto wa kipekee kuanzia muonekano wake mpaka uigizaji wake, Angelina Jolie kufungua kesi ya kudai talaka kutoka kwa mume wake Brad Pitt, sababu zikilielezwa kuwa ni ndoa yao kukosa maelewano mazuri.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, wapenzi hawa walitengana kuanzia September 15, 2016, ikiwa ni miaka miwili na mwezi mmoja tangu walipofunga ndoa yao mnamo August 2014. imeelezwa kuwa Jolie anatafuta makazi mapya kwaajili ya kuishi na watoto wao sita huku akiiomba mahakama kumpa ruhusa Brad Pitt kuwatembelea watoto wake.
Akiongea na E! News jana Jumanne, Geyer Kosinski ambaye ni Meneja wa Jolie amesema kuwa Angelina yuko tayari kufanya jambo lolote ili kuwalinda watoto wake.
TAngelina Jolie ni balozi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na masuala ya wakimbizi, moja kati ya ishu kubwa zinazojadiliwa kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa ulioanza September 19,  2016 huko New York Marekani. 

Video: DC Sophia Mjema afungua kongamano la vijana Afrika Mashariki
Dimitri Seluk: NItaongea Chochote, Guardiola Hawezi Kunizuia