Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza kufiwa na dada yake anayemfuatia anayejulikana kama Bi Mwajuma Gambo.

Ambaye alifariki dunia siku ya jana Oktoba 4, 2018 katika hospitali ya Muhimbili ambako alikuwa akipatiwa matibabu.

Aidha Gambo amesema mazishi yatafanyika siku ya Jumamosi Oktoba 6, 2018 jijini Dar es salaam kwenye makaburi ya mchikichini.

Kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika

“Kwa masikitiko makubwa natangaza kifo Cha Dada yangu mpendwa Bi. Mwajuma Gambo (akitoka yeye ni mimi) kilichotokea Jana tarehe 04/10/2018 kwenye Hospital ya Muhimbili Dar Es Salaam.

“Mazishi yatakuwa siku ya Jumamosi tarehe 06/10/2018 Saa 6 Mchana kwenye makaburi ya MCHIKICHINI Ilala Dar Es Salaam.

Amesema kwa sasa msiba upo nyumbani Kariakoo mtaa wa Mheza Karibu na Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa.

Gambo amemalizia kwa kusema ”Mwaka huu tumepata mtihani mwingine. Kazi ya Mungu haina Makosa!.” Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un.

Unafanya nini ukiwa na bosi mdogo kwako? Mambo 6 ya kuzingatia
Video: Mbunge Neema amwaga misaada Njombe

Comments

comments