Aliyewahi kuwa msanii wa maigizo wa Kundi la Sanaa la Kaole, Ramadhani Mrisho Ditopile maarufu kama Mashaka amefariki dunia katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Oktoba 20, 2018 majira ya saa 3, asubuhi.

Mashaka alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Presha pamoja na kisukari ambapo jana alizidiwa gafla na kukimbizwa hospitali ya Amana, madaktari walifanikiwa kumpa huduma ya kwanza na matibabu ikiwa pamoja na kumuwekea mashine ya kupumulia ya oksijeni.

Taarifa hizi zimethibitishwa na mtoto wa marehemu, Abdallah Ditopile ambaye amedhihirisha kutokea kwa kifo hicho na kusema baba yake aliugua ghafla usiku ndipo wakamkimbiza hospitali kwa ajili ya matibabu, Ilipofika asubuhi hali yake ikabadilika, madaktari walitupatia rufaa ya kumpelekea katika Hospitali ya Muhimbili Tawi la Mloganzila, wakati tukijiandaa kuita ambulance, akakata roho, baba ametutoka katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam.

Kwa sasa ndugu wamekusanyika nyumbani kwa kaka mkubwa wa marehemu, maeneo ya Ilala Sokoni kwa ajili ya kupanga taratibu za msiba. Baadaye wataeleza msiba utakuwa wapi, mazishi yaafanyika lini na wapi.

Treni yaua watu 60 baada ya kuvamia umati kwenye tamasha
IGP Sirro: Mo alitekwa na Silaha ya kivita yenye risasi 19

Comments

comments