Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza siku 3 za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Rais wa kwanza na Baba wa Taifa la Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe kilichotokea Septemba 6 nchini Singapore alikokuwa akipatiwa matibabu.

Hivyo basi kwa siku tatu mfululizo bendera zote nchini zitapepea nusu mlingoti, kuanzia septemba 6 hadi Septemba 8, 2019.

Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa Hayati Mugabe aliipenda Tanzania, alijenga uhusiano na ushirikiano wa karibu, kindugu na kirafiki na Tanzania tangu enzi za uongozi wa Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Julius Nyerere.

Katika hatu nyingine Wazimbabwe nao wameanza siku za maombolezo, ambapo Rais wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa ametangaza kipindi cha maombolezo cha kitaifa.

Rais huyo amesema kipindi cha maombolezo katika nchi hiyo ni hadi pale ambapo mwili wa Mugabe utakapozikwa, japo bado hajasema ni lini ambapo mwili wa Mugabe utawasili nchini Zimbabwe kutoka Singapore.

Maghembe aiomba Serikali kuingilia kati wizi wa vifurushi vya simu
Video: JPM amtaka Museveni amtumbue kigogo, Dunia yamlilia shujaa Mugabe