Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani (2017 Democracy Index) iliyozinduliwa Februari 2, mwaka huu na kuchapishwa na jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist limeitaja Tanzania kuwa ni nchi ya kwanza katika masuala ya Utawala Bora kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Hayo yamesemwa hii leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa Tanzania kuwa  nchi ya kwanza kwenye masuala ya Utawala bora imeweza kusaidia ukuaji wa Uchumi wake.

“Utawala Bora ni kigezo muhimu cha ukuaji wa uchumi na hata ustawi wa jamii, kama ambavyo Orodha ya Hali ya Demokrasia Duniani iliyotolewa na jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist imeitaja Tanzania ni ya kwanza katika ukanda wa EAC, ikifuatiwa na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC.

Amesema kuwa ripoti ya Foresight Afrika na taarifa ya Uchumi ya Benki ya Dunia vyote vimeitaja Tanzania kuwa katika nchi tano Bora za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi katika mwaka 2018, nchi hizo ni Ghana, Ethiopia, Kodivaa , Senegali na Tanzania.

Aidha, Dkt. Abbasi alisema kuwa ukuaji huo wa uchumi ni dhamira isiyoyumba ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, ikiwa ni   pamoja na kuhakikisha uchumi mkuu unaendelea kujiakisi katika maisha ya watanzania kupitia utoaji wa huduma kwa wananchi na kuboresha sekta mbalimbali.

Hata hivyo, Katika sekta ya Afya, Dkt. Abbasi amesema kuwa pamoja na ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea nchi nzima na uboreshaji wa hospitali, Serikali imetenga  bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka Bilioni 31 mwaka 2015 hadi Bilioni 269. hivyo imewezesha Serikali kuboresha  usambazaji wa dawa hadi kufikia asilimia 86 ya uhakika wa kupatikana dawa muhimu.

 

Video: Chadema yalalama kuonewa
Dkt. Nchemba ateketeza ekari sita za bangi