Serikali imekanusha vikali taarifa kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa ina mahusiano ya kibiashara na Korea Kaskazini ambayo imewekewa vikwazo vya kiuchumi na baraza hilo.

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa licha ya uhusiano uliokuwepo awali, lakini tangu mwaka 2014, Tanzania imepunguza uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi hiyo.

“Hatuna ugomvi na Korea Kaskazini, lakini kwa mpango wake wa kutengeneza makombora ya masafa marefu za nyuklia sio mzuri kwa heshima na usalama wa duniani, ndiyo maana tukaanza kuchukua hatua za kupunguza mahusiano.” amesema Dkt.Mahiga

Aidha, Dkt. Mahiga ameongeza kuwa uhusiano huo wa kibiashara ulikuwepo kabla ya vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Baraza la Umoja wa Mataifa

Tanzania na Uganda ni miongoni mwa baadhi ya nchi zinazochunguzwa na Umoja wa Mataifa kwa tuhuma za kwenda kinyume na vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.

Hata hivyo, ripoti ya uchunguzi huo ilitolewa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 9 mwezi wa Septemba. Baraza la Usalama la Umoja ikisema linachunguza tuhuma za Tanzania kuingia mikataba ya kijeshi na Korea Kaskazini inayogharimu dola za kimarekani milioni 12.5

Conte aitabiria Arsenal ubingwa
BREAKING NEWS: Singida United FC yaleta Singida United TV kupitia Azam TV