Wanamichezo waliokuwa wakichuana katika Michezo ya Afrika mwaka huu (All Africa Games 2015) wametoka mikono mitupu baada ya kufanya vibaya katika michezo mbalimbali waliyoshiriki katika fainali hizo zinazotarajiwa kumalizika kesho Jumamosi huko Kongo Brazaville.

Timu ya Tanzania iliwakilishwa katika michezo ya ngumi, riadha, judo, kuogelea, Paralimpiki (walemavu) na soka la wanawake.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Henry Lihaya,  alisema kwa njia ya simu jana kuwa wanariadha ambao walibakia wakipeperusha bendera ya nchi jana nao walishindwa kung’ara na kuifanya timu ya Tanzania kukosa medali ya aina yoyote.

“Tumeshindwa kupata medali hata moja, tunasikitika hata katika mchezo wa riadha ambao tumekimbia jana (juzi) pia tumeshindwa,” alisema Lihaya.
Alisema kati ya wanariadha wanne waliokimbia jana, Ally Khamis Gulam, ambaye aliingia hatua ya nusu fainali katika mita 200 naye hakufanya vizuri kwa kushindwa kupata nafasi ya kufika hatua ya fainali.

Alisema kwamba changamoto kubwa waliyojifunza ni timu kutoka nchi nyingine kufanya maandalizi ya muda mrefu tofauti na wanamichezo wa Tanzania na uchache wa washiriki waliokwenda kushiriki michezo hiyo.

Ukawa Wamjibu Magufuli Kutumia ‘M4C’, Wadai ‘Anatapatapa’
Amir Khan Aendelea Kumuota Floyd Mayweather