Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa Serikali ya Tanzania na Uganda, zimedhamiria kushirikiana kwa dhati katika masuala ya biashara, yenye mlengo wa kukuza uchumi.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa kutambulisha uwepo wa mkutano wa jukwaa la kwanza la biashara, kati ya Tanzania na Uganda, ambapo ameitaka Sekta binafsi, kuhakikisha inachangamkia fursa ya kuangalia ni kwa namna gani itapeleka walimu wa lugha ya Kiswahili Uganda.

”Biashara kati ya Tanzania na Uganda, imekuwa kutoka shilingi bilioni 178 mwaka 2015, hadi kufikia shilingi bilioni 358 mwaka 2018 hivyo, Sekta binafsi iangalie ni namna gani tutapeleka walimu wa Kiswahili kwenda kufundisha lugha hiyo nchini Uganda” amesema Dkt. Ndumbaro.

Aidha Serikali ya Tanzania na Uganda, zimekubaliana kuanzisha ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda kwenda Tanga, usafirishaji wa gesi pamoja na ujenzi wa reli, itakayorahisisha usafirishaji wa bidhaa hiyo kati ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili.

Video: Wakili Manyama ang'ata na kupuliza sakata la Kinana na Makamba
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 19, 2019

Comments

comments