Serikali ya Comoro imefunga shule zote katika kisiwa kikubwa cha Ngazija pamoja na viwanja vya ndege na ofisi za serikali.

Kisiwa hicho cha Comoro kinatarajia kimbunga Kenneth kupita kaskazini mwa eneo la nchi hiyo huku kikitarajiwa kuwa na upepo mkali unaokwenda kwa kasi, kilometa 200 kwa saa.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kuongezeka nguvu wakati kitakapoelekea katika pwani ya Afrika Mashariki karibu na mpaka wa Msumbiji na Tanzania.

Aidha, Kimbunga hiki kinakuja wakati Msumbiji, Malawi na Zimbabwe zikiendelea kukabiliana na maafa waliyopata kutoka kimbunga Idai kilichosababisha maafa makubwa mwezi Machi.

Kwa upande wake Msemaji wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF nchini Msumbiji, Daniel Timme amesema kuwa mashirika ya huduma za dharura yako tayari.

Pia ameongeza kuwa pamoja na Kimbunga hiki kutokuwa na nguvu kama kile cha Idai lakini kinaelekea katika jimbo la Cabo Delgado ambako sehemu kubwa ya wakazi wake ni watu wa kipato ya chini na hawana matayarisho ya kukabiliana nacho.

LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Aprili 25, 2019
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 25, 2019