Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa mpaka kupelekea viongozi mbalimbali wa taasisi kubwa duniani kuja nchini kwa ajili ya kujione na kutaka kujua mengi zaidi.

Hali hiyo imedhihirika mara baada ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang  kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip  Mpango pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Aidha, akiwa nchini, Tao Zhang atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli Ikulu Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuona ni namna gani Tanzania na IMF zinashirikiana katika kuimarisha uchumi.

Hata hivyo, Zhang atawasilisha mtazamo wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa wadau hapa nchini kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa na maendeleo endelevu, kuimarisha uchumi mkubwa (Macroeconomy) na kuwa na uchumi shirikishi.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 16, 2017
Zitto ataka hatua kali zichukuliwe dhidi ya askari polisi aliyemtishia bunduki Malima