Kwa mara ya kwanza wakulima wa mazao ya viungo mkoani Morogoro, hususan wanaolima pilipili manga na lozera, wanatarajiwa kuuza mazao yao katika soko la kimataifa baada ya kukidhi vigezo vya kulima mazao hayo bila kutumia kemikali hatarishi kwa afya ya binadamu.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa shirika la kilimo endelevu Tanzania (SAT), Janeth Maro kwenye ziara ya waandishi wa habari za kilimo hai.

“Wakulima wengi hususan kwenye maeneo ambayo mazao ya viungo yanastawi, bado hawafahamu faida zilizopo” amesema Maro.

Ameeleza kuwa kupitia zao la lozera wamepata soko zuri nchini Uswisi na ndani ya tanzania ambapo wapo kwenye hatua za mwisho kupeleka lozera iliyofungashwa katika pakiti 5000 na inauzwa kwa bei nzuri.

Amebainisha bei ya lozera kuwa pakiti ndogo ya gramu 50 inauzwa dola tano sawa na shilingi za kitanzania zaidi ya elfu kumi.

Hali kadharika ameyataja mazao mengine yanye soko nchini Uswisi ni mdarasini na pilipili manga ambapo pia wapo kwenye hatua ya mwisho kupeleka nchini humo tani 10 mpaka 15.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa Tanzania zao la lozera linastawi zaidi kwenye maeneo kama Mvomero, ambapo kuna mvua ndogo kwa mwaka na maeneo mengine yanye hali kama ya wilaya hiyo.

Meneja wa kituo cha utafiti wa kilimo hai cha SAT, Frank Mwarwa amesema lozera ni zao muhimu kwa maisha ya binadamu ambapo faida yake ina chembechembe za kuondoa sumu mwilini.

Nigeria: Gavana atangaza mapumziko siku ya kumpokea Rais
Walinzi wa G4S security mbaroni wizi wa mabilioni ya NBC