Tanzania inao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko mbadala ambayo itatosheleza kufanikisha azma yake ya kupiga marufuku biashara na matumizi ya mifuko ya plastiki.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa.

Amesema kuwa ni jambo la kushangaza kuona asilimia 100 ya mifuko ya karatasi inayotumika nchini Rwanda na asilimia hamsini nchini Kenya inazalishwa Tanzania huku Tanzania ikitumia zaidi ya asilimia 80 ya mifuko ya plastiki inayozalishwa nje ya nchi jambo linalokinzana na dhana ya kukuza uchumi wa viwanda.

“Tunao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko mbadala, wazalishaji wa mifuko hiyo wameithibitishia Serikali kuwa wanao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko hiyo ambapo Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi kimesema kitaongeza uzarishaji zaidi ya maratatu huku wawekezaji zaidi ya 50 wakiwa wameagiza mashine za kuzalishia mifuko hiyo,”Amesema Makamba.

Aidha, ameongeza kuwa nchi ya Tanzania inaweza kufanikiwa katika zoezi hilo kwa kuwa inazalisha mifuko mbadala ya karatasi ambayo hutumiwa kwa kiasi kikubwa na nchi jirani za Rwanda huku Kenya wakitumia asilimia kubwa ya mifuko kutoka Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi cha hapa nchini, Kenya ikitumia asilimia 50.

Waziri Makamba amesema kuwa wazalishaji wa mifuko mbadala wameithibitishia Serikali kuwa wanao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko hiyo ambapo Kiwanda cha Karatasi Mufindi kitaongeza uzalishaji zaidi ya mara tatu kinavyozalisha sasa huku wawekezaji zaidi ya 50 wakiwa wameagiza mashine kwa ajili ya kuzalishia mifuko hiyo.

Katika hatua nyingine Waziri Makamba alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kushirikiana kwa karibu na mamlaka zingine zitakazo husika katika zoezi la kutokomeza biashara na matumizi ya bidhaa za Plastiki zilizopigwa marufuku.

Akizungumzia marufuku hiyo Makamba amesema kuwa katika awamu ya kwanza marufuku hiyo inahusisha mifuko ya plastiki tu huku bidhaa zingine zinazotumia plastiki vifungashio vya plastiki kuendelea kutumika kwa wakati utaratibu ukiendelea.

Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni bidhaa za chakula, kilimo na dawa. Utekelezaji wa katazo hilo la matumizi ya bidhaa za plastiki nchini linafuatia utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyotoa tarehe 26, April, 2019 katika maadhimisho ya Muungano jijini Dodoma.

LIVE: Yanayojiri Bungeni jijini Dodoma leo Mei 15, 2019
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 15, 2019