Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limeomba radhi kwa wateja wake wa mikoa iliyounganishwa na gridi ya Taifa kwa katizo la umeme lililotokea leo majira ya Saa 9:00 Alfajiri.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter, TANESCO imesema kuwa sababu iliyopelekea kukatika kwa umeme ni hitilafu iliyotokea katika mfumo wa gridi.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza. Tutaendelea kutoa taarifa kadri kazi inavyoendelea. Tunawataarifu wateja wetu kuwa huduma ya umeme imeanza kurejea  kwenye baadhi ya maeneo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa na Morogoro”, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo

Hata hivyo, taarifa hiyo imeongeza kuwa wataalamu na mafundi wa shirika hilo wanaendelea na jitihada za kuhakikisha umeme haukatiki tena na unarejea kwa haraka katika maeneo yote nchini.

 

 

Dkt. Mashinji na wenzake watatu waswekwa ndani
TANZIA: Mwanasiasa mkongwe nchini afariki dunia