Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekanusha vikali taarifa inayo sambaa katika mitandao ya kijamii kuwa kutakuwa na tatizo katika mfumo wa manunuzi ya LUKU kuanzia tarehe 25 Machi 2018 hadi 05 Aprili 2018 , kwamba wateja wanunue umeme wa kutosha katika kipindi hicho.

Katika taarifa iliyotolewa na Tanesco, imsema kuwa huo ni uzushi wenye nia ya kupotosha umma kwani shirika hilo halijatoa taarifa kuhusu hitilafu katika mfumo wa manunuzi ya LUKU.

“Tunaomba wateja wote wa TANESCO waipuuze taarifa hiyo kwani haina ukweli wowote, Wateja wote mnaombwa kuendelea kutumia huduma za umeme kama kawaida,”imesema taarifa kutoka Tanesco

Meya wa Jiji la Dar aziweka kikaangoni halmashauri, azitaka zitimize makubaliano
Hukumu ya Babu Seya na Papii Kocha kusomwa kesho