Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (Talgwu) kimelaani vikali kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda cha kuwavua madaraka hadharani watumishi wa Umma na kukiita kitendo hiko ni cha kinyama.

Februari 10, 2018 watumishi wa idara za ardhi wa manispaa za Ubungo na Ilala walivuliwa madaraka hadharani hali iliyosababisha mmoja wao, Paul Mbembela ambaye ni Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Ilala kuzimia kwa muda.

”Jambo baya zaidi tunalolaani hata mtumishi huyo alipozimia Makonda aliendelea kusema Dar es salaam oyee, huu ni unyama” amesema Katibu Mkuu, Rashid Mtima.

Amesema kibinadamu mkutano huo ulipaswa kusimama kwa muda ili kumshughulikia mgonjwa.

Ameongezea kuwa chama hicho hakitetei watumishi waovu , bali taratibu zinatakiwa kufuatwa katika kuwawajibisha watumishi wanaokiuka maadili ya kazi.

”Tunalaani tunalaani sana kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa, Makonda. Sheria zinataka mtumishi anayekiuka kanuni na sheria za utumshi kushughulikiwa kwa siri hadi uamuzi wa mwisho utakapotolewa amsema Rashid.

Hayo yamezungumzwa leo Februari 13, 2018 wakati akitoa tamko la chama hicho kuhusu maamuzi yaliyochukuliwa na Mkuu wa Mkoa Makonda bila kufuata taratibu na Sheria katika kuwajibisha watumishi.

Aidha amewaasa wanasiasa na viongozi kufuata sheria wakati wa kushughulikia matatizo ya wafanyakazi.

Rabiot afunguka linalomkera PSG
Fahamu nguvu ya ndoto katika mahusiano yaliyovunjika