Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya Serikali ameongoza zoezi la kusaini mkataba na kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri, kuhusu ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Stieglers Gorge ambao unatarajiwa kuzalisha zaidi ya megawats za umeme 2100.

Makubaliano hayo yamefikiwa Ikulu Jijini Dar es salaam mbele ya viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwemo Spika wa Bunge, Jaji Mkuu wa Mahakama, Mawaziri mbalimbali wa nchi pamoja na Waziri Mkuu wa Misri.

“Tumegundua kuwa mradi huu ndio unaofaa kwa nchi yetu kwa sasa, sababu chanzo chake ni cha uhakika, kwa tathimini ya awali mradi utazalisha umeme kwa miaka 60 ijayo, na utagharimu trilioni 6.5”.amesema JPM

Aidha, amesema kuwa mradi huo utainufaisha nchi kwa kuzalisha umeme mwingi na wakutosha, hivyo kuweza kuondokana na tatizo la upungufu wa umeme.

Hata hivyo, ameongeza kuwa anafahamu kuna watu ambao wanadai kuwa mradi huo utaharibu mazingira, hivyo amesema taarifa hizo si za kweli.

 

Kitambulisho cha Ujasusi cha rais Putin chapatikana Ujerumani
Uganda kununua boti za wagonjwa wa ajali za majini

Comments

comments