Vikundi vya ufugaji nyuki vilivyopo katika halmashauri ya manispaa Tabora vimefanikiwa kuongeza kiwango cha uzalishaji asali kutoka tani 23 hadi tani52.5 na nta kutoka kilo 888 hadi  4000 katika kipindi cha januari hadi Desemba 2019.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa kitengo cha ufugaji nyuki katika halmashauri ya manispaa hiyo, Seif Salumu amesema mafanikio hayo yamechochewa na elimu hamasa uwezeshaji na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na wataalamu wa nyuki waliopo katika manispaa hiyo na taasisi nyinginezo kwa vikundi vyote vya wafuga nyuki.

Ameeleza kuwa licha elimu na mafunzo hayo vikundi 31 vilivyopo viliwezeshwa mizinga ya kisasa 2,601 na ya kiasili 3,633 na kuongezwa mizinga mingine kwa vikundi vyote vya wafuga nyuki.

Salumu amefafanua kuwa kila mazinga unatoa kilo 20 za asali hivyo kwa mizinga 420 pekee wanavuna kilo 8,400 sawa na tani8.4 za asali kwa mwaka hivyo huweza kuvuna kilo 53,500 za asali sawa na tani 53.5 kwa mizinga mingine ameongeza kuwa kwa sasa bei ya kilo moja ya asali ni 8,000 hivyo wakiuza kilo zao zote kwa bei hiyo watavuna watavuna zaidi ya sh milioni 400 kwa mwaka

Amesema kupitia mradi huo mafanikio yaliyopatikana ni makubwa na yataendelea kupatikana huku akibainisha wazi kuwa vikundi vimepata fedha za kutosha ikiwemo kuongeza thamani ya mazao yao na kuchangia uchumi wa taifa.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Komanya kitwala alitoa wito kwa vijana kuchangamakia fursa hiyo kwa kujiunga katika vikundi na kuanzisha miradi yao ya ufugaji nyuki iliwaweze kunufaika na uwezeshaji wa serikali yao

Rwanda yathibitisha mgonjwa wa Corona
Video: Mchawi wa timu asimulia "Nilitafuta Kaburi la 1995" Tuliwakuta WCB| Nikiwa Uchi wa Mnyama

Comments

comments