Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amezitaka taasisi za umma kuacha mara moja kutumia mkaa kupikia vyakula badala yake zitumie gesi kuanzia sasa.

Ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wa shughuli ya upandaji miti, katika Chuo Kikuu cha Dodoma alipokwenda kumuwakilisha Makamu wa Rais.

Amesema kuwa wakati wowote kuanzia sasa ataandika waraka na kuusambaza katika taasisi zote kubwa ikiwemo majeshi na vyuo vikuu vyote kwakuwa mamlaka hayo anayo.

“Ninayo mamlaka ya kufanya hivyo kwakuwa sheria ipo inayonipa nguvu hata kama kuna sheria nyingine inayopingana na hii itakuwa na nguvu zaidi,”amesema Makamba

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola amesema kuwa serikali haitamvumilia mwekezaji yeyote wa viwanda atakayechafua mazingira kwa kutiririsha maji machafu au kemikali kwa kisingizio cha uwekezaji.

Waliotaka kumteka Rais waandaliwa nyundo nzito
Video: Makonda amsweka ndani aliyenunua eneo la shule