Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fredrick Sumaye amesema kuwa Mzanzibar yeyote anaruhusiwa kugombea Tanzania Bara.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni, ambapo amesema kuwa watu wanaosema Salum Mwalimu hana sifa ya kugombea bara hawajui walitendalo.

Aidha, amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kiache kufanya propaganda ambazo si za kweli hivyo ni bora kushindana kwa hoja.

“Hawa akina Mtulia waache Propaganda, inawezekana hawaelewi wanachokifanya, Wazanzibar wanahaki ya kugombea popote Tanzania bara,”amesema Sumaye

Hata hivyo, ameongeza kuwa Demokrasia kwa sasa imeminywa hivyo hawapati nafasi ya kufanya mikutano ya kisiasa ingawa ni haki yao kikatiba lakini wamezuiliwa.

 

Video: Makonda amwaga chozi baada ya kukutana na Wastaafu
Uchaguzi: Chadema msiondoe macho kwenye ‘mpira’ mtamlaumu refa