Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye amesema kuwa anaiomba serikali pamoja na vyombo vyake iwe inachukua hatua za haraka pindi yanapotokea matukio ya kiharifu yanayosababisha kupoteza uhai wa watu wasiokuwa na hatia.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam mara baada ya kuaga mwili wa marehemu, Daniel John ambaye alikuwa Katibu wa Kata ya Hananasif iliyopo Jimbo la Kinondoni.

“Naiomba serikali pamoja na vyombo vyake iwe inachukua hatua kuhakikisha mambo kama haya hayatokei na pale yanapotokea basi wachukue hatua za haraka kuhakikisha wahusika wanapelekwa katika vyombo vya sheria,”amesema Sumaye

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewaachia kwa dhamana viongozi waandamizi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walioitikia wito uliotolewa na jeshi hilo siku ya jana (Jumatatu) na kutakiwa kurudi kituoni tena siku ya Jumanne wiki ijayo saa 4:00 asubuhi.

Video: Naibu Spika adai ana haki ya kikatiba kugombea ubunge
Tanzania yaongezewa tiketi kombe la dunia