Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amemuomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kutolea ufumbuzi wa mapungufu ya kikatiba na sheria juu ya suala la usimamizi wa uchimbaji wa mafuta na gesi kwa upande wa Zanzibar.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia utiaji saini wa mkataba wa ugawaji faida PSA baina ya Zanzibar na kampuni ya RAK GAS, kampuni ambayo itaendesha shuguli za uchimbaji wa mafuta na gesi Zanzibar,

Amesema kuwa mkataba huo ni batili kwani kuna mkinzano mkubwa wa kisheria na kikatiba ambao amesema usipo shugulikiwa hivi sasa ufumbuzi wake utakuwa mgumu kwa siku zijazo.

“Kwa vipengele hivyo, sheria zilizotungwa na Zanzibar kuhusiana na masuala ya mafuta na gesi ni batili mgongano wa kikatiba na ule wa kisheria kwa pamoja unaathari kubwa sana kwani sheria ya mafuta na gesi ya mwaka 2015 ya Tanzania imeeleza bayana nani ni mmiliki wa mafuta na gesi,” amesema Maalim Seif.

Aidha, ameyataja mapungufu ya kikatiba kuwa ni pamoja na Suala la Mafuta na Gesi, katiba ya Jamuhuri ya Muungano imelitaja kama suala la Muungano na sio suala la Zanzibar, na amesema ibara ya 64 kipengele cha 3 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inabatilisha Sheria iliyotungwa na baraza la wawakilishi kwa jambo ambalo ni la Muungano.

Hata hivyo, Oktoba 23, 2018 wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba huo Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein alisema mchakato huo umezingatia sheria zote za Zanzibar na si vinginevyo.

 

Ja Rule ajibu jaribio la 50 Cent kununua haki ya nyimbo zake
Paulo Dybala amuita Pogba Juventus FC