Hatimaye aliyekua nahodha na kiungo wa klabu ya Liverpool, Steven George Gerrard amejitokeza hadharani na kuwasalimu mashabiki wa klabu ya LA Galaxy baada ya kuwa shuhuda wa mchezo wa klabu hiyo wa ligi ya nchini Marekani MLS mwishoni mwa juma lililopita.

Gerrard ambaye ameitumikia klabu ya Liverpool kwa muda wa miaka 24 tangu akiwa na umri wa miaka 7, alikua katika fununu za muda mrefu za kuelekea nchini Marekani kucheza soka katika ligi ya nchini humo.

Alionekana wakati wa mchezo wa MLS pale klabu yake mpya wa Los Angles Galaxy ilipua ikipambana na Toronto FC na kuibuka na ushindi wa mabao manne kwa moja.

Gerrard anajiunga na mchezaji ambaye aliwahi kucheza kakatika ligi ya Uingereza katika klabu ya Tottenham Hotspurs Robbie Keane ambaye katika mchezo huo alifanikiwa kufunga mabao matatu.

Mashabiki wa LA Galaxy wameonyesha kufurahishwa na kuridhishwa na kitendo cha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 35 kujitokeza mbele yao na kuwasalimu, ambapo sasa wanaamini kikosi chao kitaendelea kuimarika.

Katika mtandao wa kijamii wa Twitter mashabiki wa LA Galaxy waliweka picha za mivinyo pamoja na makopo ya vilevi mbali mbali na kuzinakshia picha hizo kwa maneno yaliyosomeka ‘Welcome Steven Gerrard’.

Hii itakuwa mara ya pili kwa klabu ay LA Galaxy kumsajili gwiji wa soka kutoka nchini Uingereza, baada ya kufanya hivyo miaka minane iliyopita kwa kumsajili David Robert Joseph Beckham mara baada ya kukamilisha mkataba wa kuitumikia klabu ya Real Madrid.

Gerrard anaondoka Liverpool akiwa ameacha kumbu kumbu ya kucheza michezo 504 na kufunga mabao 120.

Riquelme: Nilifanya Makosa Makubwa Kuikataa Ofa Ya Man Utd
Chemical: Mimi Ndiye Rapa Bora Zaidi Wa Kike Tanzania